Manowari "Minerve", ambayo ilipotea miaka 51 iliyopita katika mji wa Ufaransa wa Toulon, imepatikana.
Manowari hiyo imekuwa ikisakwa kwa muda mrefu na timu ya utafutaji baharini
Kulingana na BBC, Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Florence Parly, katika ukurasa wake wa Twitter, alitangaza kwamba manowari hiyo ya Ufaransa ilipotea mnamo Januari 1968 ikiwa na mabaharia 52.
Parly ameelezea kuwa timu ya utafutaji haikuweza kuipata manowari hiyo licha yakutafuta kwa nguvu zote.
Ikumbukwe kuwa utaftaji wa manowari hiyo ulianzishwa tena mapema mwaka huu kutokana na ombi la mabaharia.
Sababu ya kutoweka kwake hakujafafanuliwa kamwe.