Na Rahel Nyabali, Tabora.
Katika kukabiliana na tatizo la mimba za utotoni ambalo limekuwa chanzo kikubwa cha kukwamisha ndoto za watoto wa kike, wadau mbalimbali wameendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na tatizo hilo lengo ni kumuwezesha mtoto wa kike aweze kupata elimu.
Akikabidhi magodoro yatakayotumika katika mambweni ya wasichana wilayani Uyui Mkoani Tabora, Naibu katibu Mkuu chama cha kutetea Haki na maslahi ya walimu Tanzania chakamwata Sospeter Ndabagoye ametoa wito kwa jamii kuona umuhimu wa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha elimu
Mkuu wa wiraya ya Uyui Gift Msuya,amesema lengo la wilaya hiyo ni kuhakikisha linaondokana na changamoto hiyo ya mimba za utotonikwa kuwatengenezea mazingira mazuri ili kuwawezesha wanafunzi kufikia malengo yao.
Aidha Changamoto ya mimba za utotoni kwa wanafunzi wa kike ambapo katika wilaya hi karibu nusu ya wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi hushindwa kuendelea na masomo ya sekondari kutokana na kupata mimba hali iliyosababisha serikali ya wilaya hii kuanzisha kampeni ya nishike mkono tuwavushe salama lengo likiwa ni kuboresha mazingira yatakayomuwezesha mtoto wa kike kupata elimu, kwa kujenga mabweni.