F Msikae mbele ya maduka yao na kuwabana - Rais Magufuli | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Msikae mbele ya maduka yao na kuwabana - Rais Magufuli


Rais Magufuli amesisitiza mfanyabiashara mdogo aliyelipia kitambulisho cha ujasiriamali asisumbuliwe na apewe ruhusa ya kufanya biashara popote nchini bila kulipishwa pesa nyingine.

Ametoa kauli hiyo leo July 11, 2019 alipozungumza na Wananchi akitokea Karagwe kuelekea Chato.

"Niwaombe pia na wafanyabiashara wadogo,msiwabugudhi wafanyabiashara wenye maduka,kwasababu wao wanalipa kodi kubwa TRA na nyie mnalipa Tsh. 20,000 ya vitambulisho, msikae mbele ya maduka yao na kuwabana," amesema.

Pia Rais Magufuli ameagiza kutolewa Lupango kwa Bwana 'Pesha' aliyekuwa akiwatoza fedha wafanyabiashara wenye vitambulisho, huku akisema amemsamehe kwani ana watoto wanaomtegemea.