Mtoto Abdul Rahman mwenye umri wa miaka kumi, Julai 12 mwaka huu alipigwa risasi ya kichwa na wanajeshi wa Israeli, kwenye kijiji cha Kufr Qaddoum kilichopo kaskazini mwa mji wa West Bank.
AbdulRahman alikua nyumbani siku iyo pamoja na familiya yake akicheza mchezo wa simu unaojulikana kwa jina la PUBG. kabla ya chakula cha mchana, Rahman alitoka nje na kwenda kucheza na wenzake. Mnamo sa nane mchana, Mtoto Abdul Rahman alipigwa risasi ya kichwa na wanajeshi wa Israel na kubebwa na ambulance kisha kupelekwa hospitali.
Kwa mujibu wa ushuhuda kutoka kwa wakazi wa kijiji, Mtoto Abdul Rahmna alipigwa risasi akiwa takribani meta 300 kutoka nyumbani kwa familia yake na hakuwa eneo ambalo wanakijiji walikua wakifanya maandamano.
Kufr Qaddoum ni moja ya vijiji vwa Wapalestina kilichopo kaskazini mwa mji wa West Bank ambao wakazi wake hutoka kila Ijumaa kuandamana na kupinga kitendo cha serikali ya Israel kufunga barabara kuu kwa zaidi ya miaka 30 sasa baada ya kujenga makazi ya wayahudi kwenye ardhi ya Wapalestina kijijini humo.
Akitoa ushuhuda kuhusu tukio hilo, Bwana Riyad Ishtaiwi mkazi wa kijiji icho ambaye pia ni miongoni mwa watu wa mwisho kumuona mtoto Abdul Rahman kabla hajapigwa risasi, amesema kwamba alimuona mtoto huyo akiwa anacheza na kisha kupigwa risasi na wanajeshi wa Israeli waliokua takribani meta200 kutoka sehem mtoto Rhman alipokuwa anacheza. Riyad aliashiria kwamba Japo mtoto Rahman hakuwa kwenye usawa wa waandamaji, wanajeshi hao walimlenga kwa risasi na hivyo masi kuonesha kwamba walifanya hivyo kwa kukusudia.
Mashuhuda walisimulia kuwa damu nyingi ilimtoka Rahman na hivyobasi alibebwa na kuwahishwa hospitali mjini Nablus ambapo alipata matibabu. Madaktari waliomtibu Rahma wamesema kwamba risasi hiyo ilipasuka ndani ya kichwa na kutengeneza vipande karibu mia moja ndani ya kichwa cha Rahman.
Akiendelea kuzungumza, Bwana Istaiwi amesema kwamba kitendo hicho kimeleta huzuni na simanzi kubwa kijijini humo. Aliendelea kusema kuwa yeye alikuwa mwenye umri wa miaka 10 pindi serikali ya Israeli ilivowanyang’anya Wapalestina archi katika kijiji hicho na kujenga makazi ya wayahudi na kisha kufunga barabara; na sasa miaka 30 baadae bado wakazi wa kijiji hicho wamenyimwa haki ya kurejea kwenye ardhi yao.
Mashhour Qaddoumi, mkuu wa harakati za Fatah katika kijiji hicho, alisema kwamba kitendo hicho cha kupigwa risasi kwa mtoto Abdul Rhman kilishtua kila mtu kijijini humo na kuleta majonzi na simanzi.
Alipoulizwa kuhusu idadi ya wakazi wa kijiji hicho waliojeruhiwa tangu maandamano hayo ya wiki kuanza alijibu, "Swali linapaswa kuwa: ni nani ambaye hajawahi jeruhiwa?"
Hata hivyo Mr Qaddoumi alisema kwamba wakazi wa kijiji cha Kufr Qaddoum wataendelea kudai haki yao na kupigania haki na ardhi yao.
Aidha Daktari Othman Bisharatkatika hospitali ya serikali ya Rafidya huko Nablus ambapo Abdul Rahman alipelekwa baada ya kujeruhiwaamesema kwamba Hali ya mtoto Abdul Rahman ni mbaya kwasababu risasi ilikuwa imepita nyuma ya ubongo. Alisema yeye mwenyewe alihesabu kati ya vipande 60 hadi 70 kwenye ubongo wa Abdul Rahman.
Hii sio mara ya kwanza wanajeshi wa Israeli kuwalenga na kuwadhurukwa makusudi watoto na hata vijana wa Palestina; Serikali ya Israel imefanya uhalifu mwingi dhidi ya watoto, na vijana wa Palestina ikiwa ni pamoja na kuwafunga magerezani mwao na kuwapa mateso ya kimwili na ya kisaikolojia.
Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kuingilia kati na kuchukua hatua dhidi ya uhalifu huu unaofanywa na Serikali ya Israel si kwa watoto na vijana wa Palestina pekeyake, bali kwa Wapalestina wote bila kujali sheria za kimataifa na Haki za Binadamu. Jumuiya ya kimataifa inapaswa pia kuweka shinikizo kwa Israeli ili kukomesha ukandamizaji na ukoloni dhidi ya Wapalestina