F Viashiria vya ugonjwa wa ini vyasababisha vijana 12 kushindwa kujiunga JKT | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Viashiria vya ugonjwa wa ini vyasababisha vijana 12 kushindwa kujiunga JKT

Takribani vijana 12 kati ya 325 ambao wamefanyiwa usaili kwa ajili ya kushiriki mafunzo ya jeshi la kujenga taifa (JKT) wamegundulika kuwa na viashiria vya ugonjwa wa homa ya ini.

Hayo yameelezwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa.

Byakanwa amefafanua kuwa vijana hao ambao wamebainika kuwa na viashiria vya ugonjwa wa homa ya ini, asilimia kubwa wanatokea Wilaya ya Nanyumbu na kupelekea kushindwa kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya jeshi, hatua ambayo imepekelea Mkoa kuamua kuwafanyia uchunguzi wa kina.

Vijana hao ambao wenye  viashiria vya magonjwa, 10 ni kutoka Wilaya ya Nanyumbu na wawili Wilaya ya Newala.

Kufuatia kugundulika kwa Visa hivyo 12 vya Viashiria vya ugonjwa wa ini Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amewataka wananchi mkoani hapa kujijengea utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kuzitambua afya zao.