Msanii wa filamu Bongo, Johari amefunguka kuhusu kashfa za wasanii wa Bongo Movie kuiba wake na waume za watu kwa kusema suala hilo halipo kwenye tasnia ya uingizaji pekee.
Muigizaji huyo amesema wale wanaoeneza hilo hawajafanya utaviti wa kutosha kwani ni vitu ambavyo vipo sehemu mbali mbali kwenye jumuiya ya watu.
"Sehemu yoyote yenye mkusanyiko wa watu mbalimbali na rika tofauti haya mambo yanatokea kwa sababu kila mtu anatabia zake" amesema.
Ameendelea kuwa sifa hizo wanasemwa wasanii wa Bongo Movie kwa sababu kwao yanaonekana zaidi, ila hata watu wengine wanafanya mambo makubwa tu.