Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa mzigo huo mpya wa jezi unapatikana kwenye Mail zote za GSM za Pugu na Msasani.
Ten alisema kuwa, ni nafasi pekee ya mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kununua jezi hizo tayari kwa ajili ya kwenda kuisapoti itakapokuwa Uwanjani Jumapili hii ikicheza na Township Rollers ya Botswana.
“Nichukue nafasi hii kuwatangazia mashabiki wa Yanga kuwa jezi mpya za timu yao tayari zipo madukani zitakazopatikana kwenye GSM Mail zote za hapa jijini Dar es Salaam,”alisema Ten.