Kuwashwa sehemu yoyote ya mwili inaweza kuwa ni matokeo ya tatizo fulani lililoko mwilini,kama vile mzio (allergy) minyoo.
Kwahiyo mwili unapowasha kunaweza kuwa ni dalili za ugonjwa unaohitaji kuchunguzwa na kutibiwa badala ya kutafuta kutibu dalili za ugonjwa.
Pamoja na hayo, kuna baadhi ya tiba za kukabiliana na tatizo hilo, ambazo ni pamoja na soya, ndimu, komamanga , unga wa ngano pamoja na majani ya ngano, lakini katika tiba zote hizo leo hii tutaelezea hii tiba ya kutumia unga wa ngano ambayo pengine inaweza kuwa ni rahisi kwa wengi.
Unachopaswa kufanya katika kutumia unga wa ngano kama tiba ni kupaka unga wa ngano sehemu zote za mwili zinazowasha na hakikisha unatumia tiba hii kwa muda wa siku 10.