F Watakiwa kuacha kuwaficha watoto Walemavu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Watakiwa kuacha kuwaficha watoto Walemavu


Na Ezekiel Mtonyole, Bahi

Wananchi wa kata ya Ibihwa wilayani Bahi Mkoani Dodoma,  wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha watoto wao ndani kwa kigezo cha ulemavu , kwani ni kinyume na haki ya mtoto, pia ni kinyume na sheria ya mtoto kifungu cha nane ikitoa katazo la jamii kumnyima mtoto haki ya kusoma kwa kigezo cha ulemavu.

Akizungumza katika mkutano na wanachi katani hapo uliyoratibiwa na shirika la International Aids service jana Wilayani Bahi mkoani Dodoma na meneja wa shirika hilo Alan Kamnde amesema ukosefu wa elimu  kwa wanachi kuhusu umuhimu wa kumthamini mtoto mwenye ulemavu bado ni kikwazo kikubwa katika jamii.

“Lengo la shirika hili ni kuhakikisha  jamii inafikiwa na kupewa uwelewa kuweza kuwaruhusu watoto kupata haki ya kielimu na Zaidi kuweza kuwajumisha watoto wenye ulemavu na wasiyo na ulemavu kujumika na kupata elimu pamoja kwasabau watoto  wote ni sawa”Amesema kamnde.

Naye Afisa Mradi wa Shirika hilo, Jane Mjidange amesema ni vyema wazazi wakawapenda watoto ,samabmba na kuomba mamlaka zinazohusika kuyashughulikia matukio ya watoto wenye ulemvu kuyachukulia uzito matukio yao.

Diwani wa kata ya Ibihwa, Daudi lesaka amesema  katika kata yake kumekuwa na mimba za mara kwa mara kesi zimefikishwa mahakani na zinafanyiwa kazi kwa mujibu wa sharia ameongeza  kwenye kata yake atachukua hatua kwa familia zote ambazo zimezuia kuwapeleka watoto shule

“Kuhusu swala la mimba tumechukua hatua za kuzipeleka kesi zote mahakamani na zinzshughulikiwa na kwa upande wa familia ambazo zimeshindwa kuwapeleka watoto shule nao tutawachukulia hatua haraka sana” amesema lesaka.