Shirika la Taifa la Mafuta la China (CNPC) ambalo linaongoza kwa uzalishaji na usambazaji wa mafuta na gesi, limetafiti hifadhi mpya ya gesi na mafuta.
Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo jana imesema, limegundua uwanja wa mafuta wenye tani bilioni 1 za mafuta katika eneo la kaskazini magharibi mwa China.
Makamu rais wa Kampuni ya PetroChina, ambayo ni tawi la CNPC Li Luguang amesema, jumla ya tani 640,000 za mafuta zitazalishwa katika eneo hilo kwa mwaka huu, na litafikia tani milioni 3 kwa mwaka katika siku zijazo.