Mtandao wa bleacherreport.com umeripoti kuwa mtanzania Hasheem Thabeet yupo mbioni kurudi kucheza ligi kuu ya kikapu nchini Marekani (NBA) akihusishwa kujiunga na timu ya kikapu ya New York Knicks.
Taarifa za Hasheem kurejea NBA zimeenea kwe baadhi ya vyombo vya habari za michezo jijini New York, kama mazungumzo na New York Knicks wakifanikiwa kumshawishi na kukubaliana nao atarejea NBA kuendeleza kipaji chake.
Hasheem amecheza NBA katika timu kama za Memphis Grizzlies, Houston Rockets, Portland Trail Blazers, Oklahoma City Thunder na Grand Rapids Drive kabla ya 2017 kujiunga na Yokohama B-Corsairs ya nchini Japan.