Mgahawa ni wazo zuri kwa kuanza mradi wa biashara, Mara baada ya kujenga na kupata imani, mgahawa utawavutia wateja bila matatizo yoyote. Lakini, kabla ya kuamua kufungua mgahawa unatakiwa kuzingatia mambo kadhaa kama vile kujenga, masuala ya leseni na kisheria pamoja na mahitaji mbalimbali yaliyowekwa na mamlaka za afya mfano TFDA kwa Tanzania. Baada ya kujaza mahitaji yote, unaweza kuanza mradi wako wa biashara katika utulivu wa muda mrefu na kwa umakini kuhakikisha unapata mafanikio.
Kama miradi mingine yoyote, eneo la biashara ni kipengele muhimu kwa ajili ya mgahawa. Chagua sehemu ambayo ni katika eneo la msongamano ambapo kuna mzunguko wa mara kwa mara na idadi kubwa ya watu.. lazima pia kuwa na maegesho mazuri ili hata wale wateja wenye vyombo vya usafiri waweze kupata eneo la kupaki vyombo vyao vya usafiri.
Huduma za Mgahawa zitolewe katika njia ya kisasa, ili kuvutia watu kutembelea na kuchunguza yaliyomo ndani yake sababu mgahawa utakuwa ukijitangaza wenyewe kwa uzuri wa huduma zake (wahudumu wakarimu, waelewa na wasio wepesi wa kuonesha kuudhika).
Aina ya vyakula na vinywaji ni lazima izingatie uhitaji wa wateja na mchanganyiko wake uwe wa kisasa. Ni lazima pia kuwa na nafasi ya kutosha katika mgahawa wako ili kutoa nafasi inayoweza kuenea wageni zaidi wakati wa masaa ya biashara. Unaweza kuweka/kuongeza eneo la bar sehemu ya wazi kwa ajili ya vinywaji ili kutoa nafasi ya kutosha kwa wateja wanaohitaji vinywaji pekee.
Kama utahitaji kuuza vileo katika bar, lazima kupata vibali muhimu kwa ajili ya matumizi ya pombe kabla ya kufungua . Pamoja na taratibu za kisheria, unatakiwa kuwa makini na mambo mengine kuhusiana na taratibu za afya.
Ni muhimu kujijengea uaminifu na kulinda afya ya wateja wako pia kwa kuzingatia maelekezo yote yanayoamriwa na idara ya afya kamavile kuhakikisha jiko na eneo la kuhifadhi chakula viko katika mahali maalum na katika hali ya usafi. Pia vyombo vinavyotumika na kila kitu kinachohusika katika mgahawa wako viwe katika hali ya usafi ikiwa ni pamoja na usafi binafsi wa wahudumu.
Daima angalia mshindani wako analenga kufanya nini au amefanya nini ili wewe ufanye ubunifu wa tofauti kuwavuta wateja wengi kwako. Kabla ya ufunguzi wa mgahawa pia ni muhimu kufahamu washindani wa karibu ambao utapambana nao kibiashara kwa ajili ya kuanzisha mgahawa wako katika namna mpya. Tathmini kabisa faida na hasara katika kusimamia kazi,maamuzi na utekelezaji wa mikakati ya biashara.