Kikosi cha Simba leo jioni kimefanya mazoezi mepesi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Kesho asubuhi kitaondoka Mwanza kwenda Musoma ili kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuwakabili Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu ambao utapigwa Jumapili Septemba 29, 2019.