Ndege ya kijeshi iliyoanguka huko kaskazini magharibi mwa Ufaransa, ilisababisha rubani mmoja kuruka na kuangukia katika nyaya za umeme.
Rubani wote waliruka katika ndege hiyo katika eneo la Brittany .
Vyombo cha habari vya kifaransa vimeripoti kuwa tukio hilo lilitokea karibu na Pluvigner.
Rubani huyo aliyeangukia umeme, sasa anaendelea vizuri na kunusurika kupigwa shoti na umeme .
Rubani wote wawili wako salama na wanaendelea vizuri.
Nyaya za umeme ambazo mtu yule aliziangukia zilikuwa na nguvu za volts 250,000, vyombo vya habari nchini humo vimetaarifu.