Na James Timber Mwanza
Kampuni ya Hisense Electronics imewataka wananchi kuwa na tabia ya kununua bidhaa za ndani zenye ubora na thamani kwa lengo la kuepukana na kununua vifaa feki vinavyotumika kwa muda mfupi, ikiwemo kusababisha hitilafu ya umeme majumbani.
Akizungumza na Vyombo vya Habari jijini Mwanza, katika maonyesho ya wafanyabishara ya Afrika Mashariki katika viwanja vya Rock City Mall, Athanas Mang'ati ambaye ni Meneja wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa, alisema kuwa vifaa bandia vya umeme vimekuwa vikigharimu maisha ya watanzania na kuwarudisha nyuma kiuchumi.
"Kampuni ya Hisense ina miaka 50 hapa nchini kisha imepewa waranti ya miaka mitatu kutokana na bidhaa zetu zilivyo bora na kukidhi viwango vinavyotakiwa, na ubaora wa hali ya juu," alisema Menneja huyo.
Mang'ati alisema kuwa ni fursa kwa wakazi wa kanda ya ziwa kufika katika maonyesho hayo kutambua bidhaa orijino zitumiazo umeme kwa matumizi bora majumabani pia zinaendana na matumizi halisi ya umeme tofauti na bidhaa bandia.
Baadhi ya wananchi waalioathirika na vifaa vya umeme vya bandia waliiomba kampuni hiyo kupanua wigo zaidi ili kuwafikia watu wengi ambao wanashindwa kutambua bidhaa zitumiazo umeme zenye kiwango kinachotakiwa.
Aidha, awali wakati akifungua maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Edwin Rutageruka, aliwaomba wananchi na wafanyabishara wenye viwanda kufika na kushiriki katika maonyesho hayo ikiwemo kutambulisha bidhaa orijino kwani serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, imefuta utitiri wa kodi kwa wafanyabishara, na kusaidia kupaa kwa uchumi.