F Wavuvi Bwawa la Nyumba ya Mungu wametakiwa kuunda Vyama vya Ushirika | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wavuvi Bwawa la Nyumba ya Mungu wametakiwa kuunda Vyama vya Ushirika


Na Ferdinand Shayo, Killimanjaro

Wavuvi wanaofanya shughuli zao katika Bwawa la Nyumba ya Mungu wametakiwa kujiunga na vyama vya ushirika vya wavuvi ili waweze kunufaika na fursa za mikopo na uwezeshaji kutoka kutoka  katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi  pamoja na taasisi za kifedha ili kuwawezesha wavuvi kutumia zana za kisasa na kunufaika na shughuli za uvuvi.

Akizungumza na Wavuvi hao, Afisa Uvuvi Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Amina Kiaratu aliyeongozana na Maafisa kutoka Wizarani ambao walitembelea vijiji vitano vinavyozunguka Bwawa la Nyumba ya Mungu Vijiji vya Handeni, Lang'ata bora, Kagongo, Nyabinda na Kiti cha Mungu kwa lengo la kuhamasisha wavuvi hao kuunda vyama vya ushirika vya wavuvi ili waweze kukopesheka

Afisa Huyo amesema kuwa Wizara  imekuja na fursa zitakazowawezesha wafugaji waweze kukopesheka na kujiendeleza kiuchumi bila kuwa na masharti magumu kigezo kikubwa cha kuweza kukopesheka ni kuwa katika vyama vya ushirika .

Msimamizi wa ulinzi wa raslimali za uvuvi ,Thobias Nyamombo amewataka wavuvi hao kuendelea kushirikiana na serikali katika kutokomeza uvuvi haramu katika bwabwa hilo ambao umekua na madhara makubwa ili kuhakikisha kuwa uvuvi unakua endelevu kwa kizazi kilichopo na kinachokuja.

Kwa upande wao wavuvi,  Joseph Solanje na Arthaur Haule wamesema kuwa wako tayari kujiunga na ushirika na wataanza taratibu kwani walikua na umoja wao wenye wanachama 200 lakini kwa sasa kutokana na hitaji la kuwa na ushirika watatumia umoja huo kufanikisha adhma hiyo ili kunufaika na fursa .