F Bondia Hassan Mwakinyo apokea cheti cha pongezi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Bondia Hassan Mwakinyo apokea cheti cha pongezi


Bondia Hassan Mwakinyo jana amepokea cheti cha pongezi toka kwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa aliyemuwakilisha Waziri Mkuu katika kongamano la Mzalendo Jasiri linalomalizika leo katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Center.

Mwakinyo amepatiwa cheti hicho kwa kuwa kijana mwenye ushawishi katika jamii na anayefanya vizuri kimichezo katika medani za kimataifa akiiwakilisha vyema Tanzania.

Bondia Mwakinyo anatarajiwa kupanda ulingoni Novemba 29 mwaka huu kupigana na Arnel Tinampey toka nchini Philippines ikiwa ni pambano lake la Kwanza la kimataifa kufanyikia nchini Tanzania.