Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, ameitembelea klabu ya soka ya KMCambapo timu hiyo imeonesha ramani ya uwanja wake.
Mwenyekiti wa klabu hiyo ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta amesema uwanja huo utajengwa eneo la Mwenge jijini Dar es salaam.
Sitta amemweleza Waziri Mwakyembe kuwa Uwanja huo utakuwa unachukua mashabiki elfu tatu na utakuwa na huduma zote za kisasa.