Na Ferdinand Shayo,Arusha
Mtendaji wa kata la Lang`ata Sabas Msofe amewajia juu baadhi ya wavuvi na viongozi wanaoshirikiana kuhujumu bwawa la nyumba ya Mungu kwa kujihusisha na vitendo vya uvuvi haramu ambavyo ni tishio kwa uvuvi endelevu.
Akizungumza katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha kata kilichowajumuisha baadhi ya maafisa wa wilaya na kueleza kuwa ametumiwa ujumbe wa simu wa kumnyamazisha asiwafichue wanaohujumu bwawa hilo na kuonya kuwa hatanyamaza kamwe.
Msofe amesema kuwa kwa sasa wanatengeneza mkakati ya kupambana na vuvi haramu katika bwawa hilo ili kuhakikisha kuwa wanatokomeza uvuvi haramu na kuwachukulia hatua stahiki wahusika.
Kutokana na changamoto za wavuvi katika bwawa hilo kaimu afisa ushirika wa wilaya hiyo bi juliana kalyoto amewataka kujiunga katika vikundi vya ushirika waweze kukopesheka ili kuwa na soko la pamoja na kuanzisha kiwanda cha kusakata samaki