Na Amiri kilagalila-Njombe
Uongozi wa kiwanda cha uzalishaji wa nguzo za umeme TANWAT mkoa wa Njombe umeahidi kuilipa serikali ya Tanzania malimbikizo ya asilimia tano ambayo kiwanda hicho kilishindwa kutoa tangu agizo la serikali lilipotolewa.
Akizungumza kiwandani hapo kilichopo halmashauri ya mji wa Njombe mara baada ya makubaliano baina ya uongozi wa kiwanda hicho na serikali, Naibu Waziri wa Tamisemi Josephat Kandege amesema uongozi wa kiwanda hicho umeahidi kutoa asilimia hiyo kutokana na kushindwa kutoa tangu serikali agizo la serikali lilipotolewa.
“Nimelazimika kufanya ziara mkoa wa Njombe mara baada ya maelekezo ya waziri mkuu katika mkoa wa Iringa ambapo tulitembelea moja ya kiwanda cha uzalishaji nguzo na kuibuka malalamiko yakionesha kuwa baadhi ya watu wanalazimika kununua nguzo Njombe na Tanga kwa sababu kuna baadhi ya tozo zimekuwa hazitozwi na Mikoa hii miwili”alisema Kandege
“Tumekubaliana na uongozi wa kiwanda TANWAT baada ya wao kukiri kutokulipa kiasi cha shilingi elfu mbili sawa na asilimia tano, na wameahidi kulipa malimbikizo ya asilimia 5 ambayo ilikuwa haitozwi tangu ambapo agizo la Serikali lilipotolewa”aliongeza Kandege
Aidha ameelekeza ujumbe pia kufika katika mkoa wa Tanga kwani serikali inataka tozo zilizopo zilipwe kwa mujibu wa sheria zitumike nchi nzima.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Cristopher Ole Sendeka amesema kiwanda cha TANWAT kilikuwa kinalipa asilimia tano ya nguzo zilizoongezewa thamani.Huku uongozi wa serikali ya mkoa umekaa na kuona ni kwa namna gani utaboresha kipato cha wananchi na kukubaliana na uongozi wa kiwanda cha Nguzo TANWAT kuwa, Licha ya kuwa nguzo watakazokuwa wanavuna kwenye shamba lao ambalo huwa wanalipa asilimia 5 baada ya kuongeza thamani.watalipa tena asilimia 5 ya nguzo ghafi wanayovuna ndani ya shamba lao.
Katika hatua nyingine waziri Kandege amekagua kwa mara nyingine ujenzi wa soko la kisasa mjini Njombe na kuona mradi huo upo katika hatua nzuri na kuwahakikishia wananchi unakamilika kwa wakati na kuona ni jinsi gani itaboresha huduma kufanya bishara hata wakati wa usiku ili huduma zipatikane muda wote kwa kuwa na aina za biashara zitakazokuwa zinafanyika ndani ya soko ili ziweze kuwa na hadhi ya Kimataifa