Na Thabit Madai,Zanzibar.
Baada ya kuibuka kwa taarifa juu ya Shirikisho la Soka la visiwani Zanzibar (ZFF) kuvunja rasmi Mahusiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Uongozi wa shirikisho hilo umekuja na kusema kuwa kwa sasa mahusinano yao yako vizuri na wanatarajia kukutana ili kutatua changamoto zilizojitokeza kati yao.
Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa wa Raisi ya ZFF Adam Natepe alisema tarifa zilizotoka Jana kwa baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii juu ya kusitisha mahusiano yao kati ya ZFF na TFF ni ya kweli ambapo kutokana na jambo hilo TFF imeitaka ZFF kukaa pamoja na kuyamaliza,ilikuondoa mzozano huo.
Alisema Shirikisho la soka Zanzibar ZFF limekubaliana na taarifa hiyo ambayo ilitolewa na shirikisho la soka Tanzania Bara TFF kukaa kikao cha pamoja na kuyamaliza mambo ambayo yaliotokea.
Alisema kweli walitoa tarifa ya kusitisha uhusiano kwa muda na ZFF lakini kwa sasa kauli hiyo imepungua uzito kidgogo hadi pale kikao kitakapo fanyika na kuyamalizika.
Aidha alisema ZFF haina tatizo na TFF lakini kwa hatua waliofikia TFF walizalimika kusitisha uhusiano na kwa hilo wamekubaliana kuyamaliza ambapo ndani ya wiki inayofata kikao hicho kitafanyika.
“Hatujui wapi kitafanyika kikao hicho,lakini tumetakiwa kuwa wiki inayokuja kkitafanyika ili kumaliziana”alisema Natepe.
Upande mwengine alisema TFF imeiambia ZFF kuwa agizo lao limekubalika juu ya timu za Tanzania bara ambazo hazijalipa deni lao ZFF juu wachezaji waliosajili Zanzibar ambapo TFF imesema imetoa muda kwa timu hizo ili kullipa madeni yao.
Kikao kati ya ZFF na TFF kinatarajiwa kufanyika muda wowote ikiwa Zanzibar au Tanzania na kikao hicho ndio kitaamua juu ya kuendelea uhusiano wao kati ya pande mbili.