ZOEZI la siku tatu la kusaka vipaji vya soka kwa vijana Zanzibar limemalizika ambapo mchezaji Nassir Abdallah Ali (BOFU) kutoka timu ya ZFDC amebahatika kupata nafasi hiyo kati ya vijana 500 waliojitokeza katika zoezi hilo.
Zoezi hilo lililofanyika viswani Humo katika uwanja wa Amani Staduim ambapo lilianza Oktoba 24 nakumalizika leo Oktoba 26 huku likiongozwa na mkocha kutoka Zanzibar na wakala wa Mchezaji wa Zamani wa Yanga na Timu ya Taifa ya Zanzibar Abdallh Shaibu Ninja ambaye anajulikana kwa jina la Alexander Marton.
Akimtaja Mchezaji huyo wakala huyo Alexander Martan alisema kati ya wachezaji vijana 500 waliojitokeza katika zoezi hilo mchezaji wa Nassir Abdallah Ali ameonesha kiwango kikubwa ambacho soka la ulaya linahitaji Mchezaji mwenye uwezo kama yeye.
Alisema kuwa ameshangazwa na vipaji vya soka kwa vijana mbali mbali ambavyo ameviona ila kwawakati huu hawezi kuwachukua vijana wote ila yupo njiani kuja kuwachukuwa na wengine ambao amewaona.
“Nimezunguka maeneo mengi lakini Zanzibar kuna vijana wadogo ambao wana vipaji vikubwa katika mchezo wa soka na tayari nmeshatoa maelekezo kwa viongozi wa soka visiwani humu ili kukuza vijana hawa wapate kuonekana” alisema Alexander Marton.
Aifahamisha kuwa Mchezaji huyo kwa sasa atamfanyia utaratibu wot wa safari ya kwenda nae Nchini Ufaransa kwa ajili ya kumtafutia timu ambayo anaweza kucheza.
Katika maelezo yake alifahamisha kuwa mara baada ya kukamilisha hatua za mchezaji huyo atarejea Zanzibar kwa ajili ya kuangalia vijana wengine ambao wanauwezo wa soka na kwenda nao kuwatafutia vilabu barani ulaya.
Nae kocha mkuu wa zoezi hilo Mohamed Salakh Richard alisema kulikuwa na chngamoto nyingi katika zoezi hilo,lakini walipambana ilikuhakikisha wanamaliza salama zoezin hilo.
Ali Mohamed Shaf alisema wakala huyo alisifu vipaji vya wachezaji huyo,huku wakitakiwa kutafuta zaidi ya 80 kukaa nao illi kuwaandaa endapo akirudi tena kuja kuja kutafuta vija wengine abmo watakwenda kuandaliwa nchini huko kwaa ajili ya soka.
Alisema kwa upande wao wamefarajika kwani watapata vjana ambao watakaiwakilsha timu ya taifa ya Zanzibar kutoka nchini mbali mbali.
“Zoezi hili kwetu nizuri maana tutapata timu ya taifa itakayo iwakilisha Zanzibar ambao watatoka nchi mbali mbali”alisema.
Nassir Abdalla ambae alipta nafasi hiyo alisema awali alikatishwa tama,lakini alirudi tena kwa mara ya pili na kuonesha kipaji chake ndipo alipofakiwa,hivyo aliwataka vijana wenzake kutokata tama kwa maneno ya watu