Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako leo Septemba 30, 2019 amefungua kiwanda cha kutengeneza samani cha Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Dodoma
ikiwa ni pamoja kutunuku vyeti wahitimu chuo hicho katika mahafali ya 36 yaliyofanyika jijini Dododma.
Kiwanda hicho kimejengwa kwa zaidi ya sh bilioni 3 ikiwa ni gharama za ujenzi, ununuzi na ufungaji wa mashine na mitambo ya karakana.
Kiwanda hicho kitakuwa kikitumiwa na wanafunzi kama sehemu ya mafunzo na kuzalisha bidhaa mbalimbali za mbao ikiwa ni hatua ya kuipeleka nchi kwenye uchumi wa Kati kupitia viwanda.
Halfa hiyo imehudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Juma Nkamia na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.