F China, Ufaransa zasaini mikataba ya kibiashara | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

China, Ufaransa zasaini mikataba ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa China Xi Jinping wametangaza leo kusaini mikataba mikuu ya kibiashara mjini Beijing ya kiasi cha thamani ya dola bilioni 15.

Mikataba iliyosainiwa ni ya sekta za usafiri wa angani, nishati na kilimo. Kampuni 20 za Ufaransa zilipewa idhini ya kuuza nyama ya kuku, ng'ombe na nguruwe nchini China.

Macron na Xi wametangaza mikataba hiyo katika kikao cha wanahabari kama sehemu ya ziara ya kiongozi huyo wa Ufaransa nchini China.

Habari hizo zimekuja wakati kukiwa na ongezeko la mivutano ya kiuchumi kati ya China na Marekani.

Xi amesema katika taarifa kuwa viongozi hao wawili wametuma ujumbe thabiti kwa ulimwengu kuhusu umuhimu wa kuhimiza ushirikiano wa kimataifa na biashara huru pamoja na kushirikiana katika kujenga demokrasia za wazi.

Aidha, Viongozi hao wawili walitoa taarifa ya pamoja wakielezea kuunga mkono Mkataba wa Paris kuhusu Mazingira uliotiwa saini 2015 wakiutaja kuwa usioweza kubatilishwa.

Marekani ilianza rasmi mchakato wa kujitoa rasmi wiki hii.