Chia seeds ni mojawapo ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha virutubisho. Mbegu za chia zina virutubisho mbalimbali ambavyo ni muhimu kwa afya ya mwili na ubongo. Mwili ni rahisi kupata virutubisho vyote vilivyomo katika mbegu hizi kwani zinameng'enywa kwa urahisi sana.
Historia ya chia seeds Mbegu hizi zinatokana na mmea unaojulikana kitaalam kama SALVIA HISPANICA, mmea huu unapatika sana Amerika ya kusini japo siku za hivi karibuni zao hili linalimwa hapa nchini Tanzania mikoa ya Morogoro na Karagwe(Kagera).
Mbegu hizi tokea zamani zimekua zikitumiwa kama chakula na dawa ya magonjwa mbalimbali na makabila ya AZTECS na Mayans yote kutoka Amerika ya kusini. Chia ni neno la Lugha ya Wa AZTEC likiwa na maana ya nguvu. Inasemekana kwamba kijiko kimoja cha mbegu za chia zilikuwa zinaweza kuwafanya watu kukaa masaa 24 bila kuhitaji chakula kingine,hivyo zao hili lilikua likitumika sana kwa askari ili kuwasaidia kuwapa nguvu na kustahimili magonjwa mbali mbali.
Virutubisho vilivyo ndani ya mbegu za chia Sababu ya mbegu kuwa na umuhimu katika afya ya mwili ni kutokana na kiwango kikubwa cha virutubisho vilivyomo ndani yake. Mbegu hizi zina kiwango kikubwa cha omega- 3, Vitamini,proteini na madini. Gram 28 za chia zinakua na virutubisho katika kiwango kifuatacho FIBER- 39 gm PROTINI- 14 gm MAFUTA- 32GM (18 gm ikiwa ni Omega 3, na 6gm Omega 6)
Madini kwa kiwango kinachohitajika kwa siku Calcium- 64% Manganese- 107% Magnesium-107% Phosphorous - 96% Pia mbegu hizi zina Vitamin A,B,D na E, Madini joto kama Iron,Iodine,niacine, thymine na kemikali za kulinda mwili ( antoxidants)
Faida za chia seeds kiafya Tafiti zinaonesa kwamba unapotumia mbegu hizi mara kwa mara inaweza kuimarisha afya ya mwili wako na kukukinga na magonjwa mbalimbali.
Zifuatazo ni faida za matumizi ya mbegu hizi.
Kulainisha ngozi na kupunguza dalili za uzee (skin and aging)
Tafiti zinaonesha kwamba ndani ya mbegu hizi kuna kemikali zinazosaidia kupunguza makali ya radikali huru (free radicals) zinazotengenezwa mwilini mwetu na kuleta matatizo mbali mbali kwenye ngozi. Kemikali hizi zinajulikana kama phenolic ant oxidants. Na kulingana na tafiti Mbegu za chia ndo chakula chenye ant oxidants nyingi kuliko vyakula vingine.
Antoxidants zinasaidia kutengeneza seli mpya za ngozi na kuondoa zile zilizokufa hivyo kuzuia ngozi kuharibika na kuwa na makunyanzi,Pia kutumia mbegu hizi inasadia kuepusha seli za ngozi kufa kabla ya muda wake kutokana na magonjwa.
Mfumo wa kumeng'enya chakula (digestive system) Mbegu za chia zina kiwango kikubwa cha Fibers. Kwa kijiko kimoja unapata 11gram za fibers. Kama tunavyojua fibers zinasaidia sana katika kumeng'enya chakula. Pia Taasis ya Ugonjwa wa kisukari nchini marekani (AMERICAN DIABETIC ASSOSIATION), Na shirika la afya nchini Uingereza (NATIONAL HEALTH INSTITUTE) wanasema kuwa mbegu za chia zinasaidia kubalance kiwango cha sukari mwilini hivyo zina faida kwa wagonjwa wa kisukari.Kutokana na kiwango kikubwa cha fibers ambazo zinasaidia kongosho kuzalisha Insulin ya kutosha.
Mbegu hizi zina LINELONIC ACID ambayo inausaidia mwili kufyonza VITAMIN A,B,D na E kutoka kwenye vyakula.
Fibers pia zinasaidia kuimarisha kuta za utumbo Hivyo kusaidia kuondoa tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu sana (Constipation).
Mbegu hizi zinasaidia kupunguza uzito kwa watu wenye uzito uliopita kiasi kwani tafiti zinaonesha kwamba mbegu hizi ziwapo tumboni husharabu maji na kuvimba hvyo kumfanya mtu ajisikie ameshiba ndo maana tafiti zinasema mbegu za chia ni nzuri kuondoa njaa ( hunger suppresser) hivyo nzuri kwa watu walio katika program ya kupunguza uzito ( Diet).
Pia mbegu hizi zinapovunjwavunjwa hutengeneza kitu kama mafuta (gel) kinachosaidia kukua kwa wadudu wanaosaidia kumeng'enya chakula waliopo tumboni (prebiotic)
Afya ya moyo Mbegu za chia zinasaidia mwili kubalance kiwango cha Lehemu (cholesterol) na kupunguza hatari ya mtu kupata tatizo la mishipa ya damu kujaa mafuta(Atherosclerosis) na kupelekea tatizo la shinikizo la damu kuwa juu, Hivyo mbegu hizi ni muhimu katika kuimarisha afya ya Moyo na kuondoa hatari ya kupata Tatizo la shinikizo la damu kuwa juu.
Hii ni sehemu ya majibu ya utafiti kuhusu Mbegu za Chia na matatizo ya moyo: The available human and non-human studies show possible effectiveness for allergies, angina, athletic performance enhancement, cancer, coronary heart disease (CHD), heart attack, hormonal/endocrine disorders, hyperlipidemia, hypertension, stroke, and vasodilatation. Some evidence also suggests possible anticoagulant, antioxidant, and antiviral effects of Salvia hispanica.
Afya ya ubongo Chia seeds zina kiwango kikubwa cha Omega -3 na Omega- 6 Fatty acids ambazo ni muhimu sana katika kusaidia ubongo kutengeneza seli zake. Virutubisho hivi ni muhimu sana kwa watoto.chia ni mmea pekee wenye virutubisho hivi.
Kutibu na kukinga kupata ugonjwa wa kisukari Watafiti kutoka chuo -University of Litoral, Argentina katika utafiti wao waliona kuwa Mbegu hizi zina Alpha Linolenic acid na Fibers nyingi, vitu hivi vinasaidia kupunguza mafuta kwenye damu (excessive fat in the blood) na kuzuia tatizo la mwili kushindwa kutumia Hormone ya insulin ( Insulin resistance) hali inayopelekea kisukari aina ya pili (type 2 diabetes ).
Kuupa mwili nguvu Tafiti zilizochapishwa kwenye jarida la Journal of Strength and Conditioning zinasema kuwa matumizi ya mbegu za chia huupa nguvu mwili mara mbili ya jinsi vinywaji vya kuongeza nguvu kama lucozade vinavyoweza kuongeza nguvu ya mwili. Pia mbegu hizi zinaongeza body metabolism hivyo mwili unatumia mafuta kama chanzo cha nguvu hivyo kusaidia kuondoa kitambi.
Kuimarisha mifupa Kama tulivyoona mbegu hizi ndani yake kuna kiwango kukubwa cha Madini ya calcium hivyo husaidia kuimarisha mifupa, pia husaidia kuwakinga watoto na tatizo la matege.
Saratani ya matiti na shingo ya kizazi Utafiti unaonesha kuwa Kemikali ya alpha linolenic acid inasaidia kuzuia utengenezwaji wa seli za saratani ya Matiti na saratani ya shingo ya kizazi. Hivyo matumizi ya mbegu hizi husaidia kuwaondoa kina mama katika hatari ya kupata saratani hizi.
Afya ya meno Kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya calcium, phosphorous, vitamin A na zinc mbegu hizi zinasaidia kuimarisha afya ya meno pia.
Ujauzito Matumizi ya mbegu hizi wakati wa ujauzito inasaidia kumpatia mama virutubisho muhimu vinavyohitajika kipindi cha ujauzito na muhimu katika ukuaji wa mtoto mfano Omega -3.
Jinsi ya kutumia mbegu hizi Unaweza kuzitafuna mbegu hizi Unaweza pikia kwenye chakula chako kama mchuzi wa samaki nyama au kuku Inafaaa kuchanganya kwenye uji ,maziwa ,juice maziwa mgando, smoothies, fruit salad, vegetable salad etc Unaweza nyunyiza juu ya chakula chako wakati wa kula kama wali ndizi supu n.k
Kama unazitumia kwa lengo la kupunguza uzito Asubuhi kabla ya kula chochote weka vijiko viwili vya chakula kwenye kikombe weka maji ya moto ukipenda kamulia limao. Kunywa mchanganyiko huo. Itakupa nguvu na kukushibisha kunywa chai yako baada ya nusu saaa au zaidi.
Pia kabla ya kula chakula una changanya kijiko kimoja kwenye glass moja ya maji acha itulie kwa nusu saa ndio unywe. au kama unaweza unatafuna kijiko kimoja cha mbegu hizi unatulia nusu saa ndio unakula
Kwa watoto Unaweza kumchanganyia mtoto kwenye uji,juice, maziwa nk. pia unaweza kuzisaga mbegu hizi pamoja na viungo vingine vya unga wa lishe au ulezi.
Mbegu hizi kwa sasa zinapatikana hapa nchini kwetu.endapo unahitaji mbegu hizi na hujui wapi pa kuzipata wasiliana na namba hii 0762167811 au 0719431888 utaelekezwa wapi unaweza kuzipata.