Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai hapo jana Jumanne aliupokea na kufanya mazungumzo na ujumbe wa maafisa wa Bunge la Kenya wakiongozwa na Katibu msaidizi mwandamizi, Lawrence Amollo aliyeambatana pia na Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, Mahusiano na Machapisho, Njenga Ruge walipotembelea ofisini kwake jijini Dodoma.