F Njombe watakiwa kuzingatia lishe kukabiliana na udumavu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Njombe watakiwa kuzingatia lishe kukabiliana na udumavu



Na Amiri kilagalila-Njombe

Tatizo la watoto kupata udumavu mkoani Njombe linatajwa kuchangiwa na tabia za mfumo dume ambapo wanaume wamekuwa wakiwanyima fedha za matumizi wanawake kwa ajili ya kununua chakula bora ,ulevi kwa wanawake na wanaume ,pamoja na kutozingatia milo mitatu kwa siku.


Pamoja na sababu hizo wanawake wa kijiji cha Matola mkoani Njombe, wakati wa maonesho ya afya na lishe yaliyofanyika kijijini, hapo wamelalamikia ushirikiano mdogo kutoka kwa wanaume kwa madai kuwa wanaume wamekuwa hawashiriki katika huduma za afya zinazo husu mama na mtoto na kuwaachia wanawake majukumu ya malezi.

“Mala nyingi wababa hawafuatilii sana watoto wanawaachia tu akina mama utakuta wanaenda sehemu za starehe hata hawafuatilii maendeleo ya watoto’alisema mmoja wa akina mama.


Msimamizi wa afya ya msingi kata za Matola na Makowo Ignasi Mligo amesema kuwa maadhimisho hayo yamefadhiliwa na mashirika ya cuam na tahea chini ya mradi wa tubadilishe ya kilenga kuendelea kukabiliana na tatizo la udumavu ambalo linawakabili watoto wengi mkoani Njombe kwa asilimia 56.

“Watu wako bize na majukumu yao hawaangalii mambo ya msingi yanayohusu huduma za watoto na hasa kweny mpango wa mlo umekuwa ni hafifu kabisa hapa Njombe,lakini wamesahau kwamba swala la watoto ni jambo la msingi mno”anasema Ignasi Mligo.


Wadau wa elimu wanasema kuwa upo umuhimu mkubwa wa kuzingatia afya,malezi na lishe kwa watoto tangu mimba inapotungwa kufuatia madhara wanayokutana nayo kwa watoto waliodumaa ambapo huwa ni ngumu kuelewa wanapo fundishwa.


Mgeni rasmi katika maonesho hayo ya afya na lishe mganga mfawidhi wa zahanati ya Kijiji cha Mbega kata ya Matola halmashauri yamji wa Njombe ameonya vikali matumizi ya pombe kwa wazazi pamoja na tabia ya kutozingatia milo.