F Yanga yamtangaza rasmi Katibu Mkuu wa klabu hiyo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Yanga yamtangaza rasmi Katibu Mkuu wa klabu hiyo

Uongozi wa Klabu ya Yanga umemtangaza rasmi David Ruhago kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo kuanzia leo tarehe 11/11/2019. 

Taarifa iliyotolewa leo na Afisa Habari wa Yanga, imesema uteuzi huo umefanywa na kamati yake ya utendaji chini ya Mwenyekiti Dkt. Mshindo Msolla.