Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad amekanusha taarifa zilizodai kuwa alikuwa ametekwa.
Akizungumza na Azam TV, Prof Assad amesema siku ambayo inadaiwa alichukuliwa na watu wasiojulikana, alikuwa kwenye hafla ya kidini wilayani Kisarawe.
"Kilichotokea nadhani ni kutoelewana tu, mimi nilialikwa na taasisi moja inayoitwa TANPO, kule nilipokwenda ilikuwa mbali sana, kuna changamoto ya kuwepo kwa mtandao, lakini mimi nilikuwa sawa kabisa" amesema Profesa Assad.
Aidha Prof. Assad amewataka watu kueleza jambo kama wanaliona haliko sawa, na si kulikalia kimya ili kuondoa sintofahamu.