F Mbunge wa Ilemela aagiza halmashauri kuondoa mkanganyiko utoaji mikopo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mbunge wa Ilemela aagiza halmashauri kuondoa mkanganyiko utoaji mikopo



Na James Timber, Mwanza

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amekea urasimu na uzembe unaofanywa na baadhi ya wataalamu wa idara ya maendeleo ya jamii katika zoezi la utoaji wa mikopo ya vikundi vya vijana, wanawake na walemavu inayotolewa na halmashauri nchini ikiwa ni utekelezaji wa sheria inayotaka kutengwa kwa asilimia kumi ya mapato ya ndani kwaajili ya mikopo hiyo ambapo 4% inatakiwa ikopeshwe kwa vikundi vya vijana, 4% vikundi vya wanawake na 2% kwa vikundi vya walemavu bila riba.

Akizungumza na vikundi kutoka kata za Kirumba, Ibungilo, Kitangiri na Nyamanoro Mhe Dkt Angeline Mabula amewataka wataalamu wa idara ya maendeleo ya jamii kuwaelimisha wananchi kabla ya kuwapa mikopo hiyo sanjari na kuondoa urasimu usio wa msingi wa kuwataka wananchi kuwafata maofisi badala ya hao kuwafata wananchi na kuhakikisha kuwa maafisa wa kata wanasikiliza na kuzipatia ufumbuzi changamoto ndogo ndogo zinazoletwa na wananchi maofisi kwao kuliko kuwasumbua wananchi kwa kuwasukimia watendaji wa ofisi kuu za wilayani

'.. Niagize maafisa maendeleo ya jamii wa kata mtimize wajibu wenu kwasababu haiwezekani kila shida mwananchi atembee mpaka buswelu makao makuu kufata ufumbuzi wakati nyie mpo na mnalipwa fedha za Serikali kwa kazi hiyo ..' Alisema

Aidha Mbunge huyo amewaahidi wananchi hao kuendelea kushirikiana na Serikali na taasisi binafsi kuhakikisha wananchi hao wanaendelea kupata elimu ya ujasiriamali na mikopo nafuu kama utaratibu wa ofisi yake unavyofanya miaka yote huku akiwashukuru madiwani wa viti maalumu na viongozi wengine wa Serikali na chama cha mapinduzi kwa ushirikiano wanaoutoa na usimamizi mzuri katika zoezi hili la utoaji wa mikopo huku akivitaka vikundi vinavyokopa kuhakikisha vinarejesha ili kutoa fursa kwa wengine kukopa.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Ndugu Shukran Kyando amesema kuwa mpaka sasa zaidi ya milioni 600 imetolewa na ipo kwenye mzunguko kama mkopo huku zaidi ya milioni 500 ikitegemewa kuongezwa hivi karibuni kutimiza zaidi ya bilioni moja kama jumla ya mkopo wote uliotolewa huku akivitaka vikundi vyote vyenye changamoto ya mkopo vilivyolalamika kupitia mkutano huo kufika ofisini kwake siku ya jumatatu kwa utatuzi.