Serikali yawataka wananchi kuwekeza katika kilimo cha Mboga mboga na Matunda


Na. Baraka Messa Songwe

Wizara ya kilimo imewataka wananchi na wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali mkoani Songwe  kuwekeza kwenye kilimo cha mbaoga mboga na matunda ili kutataua chanagamoto ya utapiamlo na udumavu unao ukumba mkoa wa Songwe hivi sasa.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Kilimo,  Japhet Hasunga wakati akiongea na viongozi wa mkoa wa Songwe katika ziara yake ya siku mbili, akizungumzia kuhusiana na hali ya chakula na jitihada za Serikali kuhakikisha uzalishaji wa chakula unaongezeka kutokana na kuboreshwa kwa masoko ya ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa mkoa wa Songwe ni miongoni mwa mikoa ambayo imebalikiwa kwa kuwa ardhi nzuri yenye uwezo mzuri wa kustawisha mazao mbalimbali yakiwemo ya mbogamboga na matunda ambayo ni muhimu katika kujenga miili.

Waziri Hasunga alisema pamoja na mkoa kuzalisha kwa wingi mazao ya chakula lakini kilimo cha mbogamboga na matunda kimekuwa hakitiliwi mkazo na wakulima wengi mkoani humo licha ya mkoa kusheheni mito mingi ambayo inafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

"Wakulima wengi ndio wanaokumbwa na changamoto ya watoto wao kuwa na upungufu wa lishe hii ni kutokana na kukosa mlo kamili, ukienda hapo kwenye hospitali teule ya mkoa wa Songwe utawakuta wakulima wengi ndio wanateseka na magonjwa ya upungufu wa Lishe ,

tumekisahau sana kipengele hiki muhimu cha kilimo cha mboga mboga na matunda ambacho ni muhimu kwa ajili ya kujenga miili yetu na kutuingizia kipato chetu '' alisema Hasunga.

Aidha Waziri Hasunga amemtaka mkuu wa Mkoa wa Songwe kuwahamasisha wakulima wa Songwe na wawekezaji kutoka nje kuwekeza katika kilimo hicho chenye tija  ili kutatua hali ya udumavu inayoukumba mkoa wa Songwe .

Aliongeza kuwa mlaka ya husika kuanzia hivi sasa itakuwa inakusanya takwimu za kilimo cha mboga mboga na matunda ili kuishindanisha mikoa yote nchinini lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji na kuimalisha afya za watanzania ili kupata makundi yote ya vyakula vya kujenga mwili na kulinda mwili.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Songwe, Bridedia Nicodemas Mwangela alisema kuwa mkoa wa Songwe pamoja na kuwa mkoa wa tatu kwa uzalishaji nchini lakini bado haufanyi vizuri katika kipengele cha matumizi bora ya chakula bora nakupelekea kuwa na udumavu mkubwa kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano.

 Mwangela alisema wamejipanga kutoa zawadi kwa mkulima bora katika maazimisho ya siku ya Kimondo  ambayo huazimishwa kidunia  juni 30 kila mwaka lengo likiwa kuhamasisha zaidi uzalishaji wa mazao mbalimbali mkoani Songwe.