F Serikali yazindua mradi wa ujenzi DIT Mwanza, kugharimu Tsh. Bilioni 37 | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Serikali yazindua mradi wa ujenzi DIT Mwanza, kugharimu Tsh. Bilioni 37


Serikali imezindua mradi wa ujenzi wa majengo mapya ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kampasi ya Mwanza wenye thamani ya Sh. Bilioni 37 unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (World Bank).

Uzinduzi huo umefanywa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha sambamba na mahafali ya kwanza ya Taasisi hiyo katika kampasi ya Mwanza ambapo amesema ujenzi huo utaanza karibuni na unatarajiwa kukamilika Desemba 2024.

Ole Nasha ameongeza kuwa mradi huo utaongeza udahili kwa zaidi ya asilimia 50 katika fani mbalimbali za ufundi na teknolojia na utawezesha kuhuisha mitaala katika fani ya ngozi ili kuzalisha mafundi mahiri watakaoweza kujiajiri na kuajiriwa.