Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo kutoa agizo kwa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), Mkoa wa Dar es Salaam kutengeneza mashimo na viraka vyote kwenye barabara ndani ya jiji hilo.
Meneja wa TARURA mkoa wa Dar, Mhandisi Chacha Magori amesema hivi karibuni wataanza ukarabati wa barabara hizo sambamba na ujenzi wa barabara mpya kwenye mitaa mbalimbali wilaya ya Ilala.
Amesema mpango huo utazihusu barabara chakavu katika maeneo ya Kariakoo, Upanga Magharibi, Mchikichini na Ilala.