Na Thabit Madai,Zanzibar.
Waziri wa Vijana,Utamaduni, sanaa na Michezo Zanzibar Balozi Ali Karume amekabidhi bendera kwa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar herous) ambayo inatarajiwa kusafiri kesho kuelekea Nchini Uganda kwa Mashindano ya Cecafa Seniors Challenge Cup yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 07 mwezi huu.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Paradise iliyopo Uwanja wa Amani Mjini Magharib Unguja.
Akikabidhi bendera Waziri hiyo aliwaambia wachezaji wa Timu hiyo ya Taifa kuwa wanatakiwa kwenda kuonesha ushindani wa hali ya juu katika mashindano na kurudi na ubingwa kwani wazanzibar wanawategemea wao.
“Wazanzibar wanamatarajiio makubwa na wao hivyo nakuombeni mukashindane na si kushirikia katika mashindano hayo”alisema Waziri Karume.
Katika maelezo yake Waziri huyo waliwataka wachezaji hao kusikiliza kwa makini maelekezo watakayopewa na viongozi wa timu hiyo kwa lengo la kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Aliwaambia watakiwa kwenda kucheza michezo kwa kwanidhamu ya hali ya juu ili kuitangaza vyema Zanzibar katika ulimwengu wa soka.
“Mchezo wa mpira wa mguu unakwenda sambamba na utamaduni wa Nchi hivyo ni busara kucheza michezo yenu kwa nidhamu ya hali ya juu na kucheza michezo kwa vurugu au utovu wa nidhamu” alisema Wazirii huyo.
Upande wake Nahodha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar,Mudathir Yahya aliahidi kufanya viuri katia mashindano hayo na kurudi na Ubingwa.
“kwa leo sina mengi ila tunawaahidi wazanzibar kuwa tunakwenda vitani kupambana na kurudi na Ubingwa kwa mwaka huu” alisema Mudthir Yahya.
Nae katibu Mkuu wizara ya Vijana,Utamaduni, sanaa na Michezo Zanzibar Omari Kingi alisema wizara tayari wameshaandaa utaratibu mzima wa safari ya timu ya kwenda na kurudi.
“Tayari tumeshakamilisha safari ya timmu yenu kama Rais wa Zanzibar alivyotuagiza kusimamia timu hii ya taifa na kesho Asubuhi atasafiri kuelekea nchini Uganda” alisema Katibu Mkuu huyo
Katika Mashindano Zanzibar imepangwa kundi moja na Tanzania Bara (Kilimanjaro stars),Kenya ambao ndio mabingwa watetezi pamoja na Djibouti.