Na Thabit Madai,Zanzibar.
Wadau wa kupambana na vitendo vya udhalilishaji kwa watoto Zanzibar,wamesema kwamba kushamiri kwa vitendo vya udhalilshaji pamoja na Mmong’onyoko wa maadili kwa watoto wadogo husababishwa na athari za utandawazi katika jamii.
Wamesema kwamba uwepo wa utandawazi katika jamii ni chanjo kikubwa cha Mmong’onyoko wa maadili ambapo hivi sasa watoto wadogo wanaripotiwa kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na mila na utamaduni wa kizanzibar.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati ya kupambana na vitendo vya udhalilishai kutoka Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA), Sheikh Ali Abdallah Amour wakati akizungumza na Mwanishi wetu kuhusu mapambano dhidi ya Udhalilishaji kwa watoto visiwani hapa.
Mahojiano hayo ni katika kutekeleza Mradi wa kutetea watoto visiwani humu ambao unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulukia watoto Duniani UNICEF na kutekelezwa na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA).
Katibu huyo alisema kwamba kushamiri kwa kasi vitendo vya udhalilishaji hasa kwa watoto kwa watoto ni matokeo ya athari za utandawazi katika jamii.
Alieleza kuwa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar imefanya tafiti nyingi juu ya kuwepo kwa Mmongonyoko wa maadili kwa watoto visiwani Zanzibar na kubaini kuwa watoto kwa watoto hufanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili kutokana na kuwepo kwa utandawazi.
“Tulipo pita katika Shehia pamoja na maskulini tulibaini kuwepo kwa vitendo vya watoto kwa watoto wakiwa wanalawitianiana, na tulipoatafuta sababu hasa tulibaini ni matokeo ya utandawazi” alieleza katibu huyo Sheikh Ali Abdallah Amour.
Aliongeza kuwa katika tafiti hizo kikubwa walichokiabaini kuwa watoto wadogo wanalawitiana pamoja na kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili kutoana kuwa wanaona na kuiga kutoka katika filamu za kimagharib ambazo wanaziona takribani kila siku.
“Watoto wameona katika michezo kisha wao wanaiga michezo hiyo, kikubwa utandawazi kuwa free ndo maana hupelekea jamii yetu kukuwa na vitndo visivyo faa” alieleza.
Alieleza kuwa athari inatokea zaidi kwa watoto wa kiume ambapo wanapoiga michezo hiyo na kupelekea kulawitiana ambapo kusababisha watoto kuwa kuharibika na kuwa katika hali ambayo ni tofauti na maumbile yake.
“Ili kupigana vita dhidi ya vitendo hivi jambo la mwanzo ambalo tunatakiwa kuanza nalo ni kuwepo kwa utandawzi ambao kwa sasa umekuwa kwa kiasi kikubwa nawahanga wakubwa ni hawa watoto wetu” alisema
“Mimi naumia na hawa watoto wa kiume kwanza ukiangalia hawa watoto wakiume ni wadogo idadi ndogo sana ukilinganisha na hawa watoto wa kike sasa vitendo hivi hupelekea kuwabadili watoto hawa kimaumbile na kuwa kama wanawake, hili taifa linaelekea wapi” alieleza Sheikh huyo.
Alisema Serikali inatakiwa kupiga vita suala zima la utandawazi pamoja na kuwepo kwa picha ambazo haziendani na maadili ya kizanzibar.
“Kiukweli hizi picha watoto wetu wanaona kisha wanaiga na kupelekea jamii kukukua katika maadili yasiyofaa pamoja na kukosa nguvu kazi kwa vizazi vijavyo” alisema Sheikh huyo.
Alifahamisha kuwa wao kama jumuiya ya Maimamu katika kukabiliana na tatizo hilo wameanza kutekeleza mpango maalumu wa kuanzisha vyuo vya ndoa kwa lengo la kuwafamahisha wanandoa wa baadae nana ya maelezi na kuepuka athari za utandawazi katika jamii.
Nae Halima Kassimu Mohamed kutoka Jumuiya hiyo ya Maimamu Zanzibar, alisema kwamba kushamiri kwa vitendo vya udhallishaji kwa watoto wadogo visiwan humu inatokana na jamii kuacha kuishi kwa kufuata mienendo ya dini pamoaja na mila na tamaduni zao.