F Baraza la madiwani Kigoma kupeleka Takukuru Ubadhirifu wa fedha zaidi ya million 800 | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Baraza la madiwani Kigoma kupeleka Takukuru Ubadhirifu wa fedha zaidi ya million 800

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji limekaa kikao na kupitisha agenda mbalimbali zilizohusiana na ubadhilifu wa fedha Zaidi ya milioni mia nane.

Hayo yamebainishwa jana katika kikao cha baraza hilo ikiwa ni kujadili na kubainisha jinsi ambapo fedha zimetumika vibaya mara baada ya ukaguzi kufanyika katika Manispaa hiyo.

Ubadhilifu huo umetokea mara baada ya baadhi ya viongozi wasio waaminifu kushindwa kusimamia miradi mbalimbali katika manispaa hiyo ikiwemo ujenzi wa maabara za sayansi,ujenzi wa vituo vya bajaji,na upangishwaji wa nyumba katika manispaa hiyo.

Aidha katika ubadhilifu wa shilingi million mia tatu hamsini kwa uuzwaji wa viwanja katika manispaa bila taarifa serikalini baraza la madiwani limeamua suala hilo lipelekwe katika kitengo cha uchunguzi TAKUKURU.

Pia Halmashauri ya Manispaa Kigoma ujiji kuuza kiwanja no 295 barabara ya Lumumba kisichokuwa na umiliki wake ambapo aliye kuwa mtumishi wa umma Athumani Juma amefunguliwa kesi ya jinai na fedha za kiwanja hicho kimelipiwa million hamsini kwa mwenye kiwanja hatimaye mpaka sasa kiwanja hicho kinamilikiwa na Manispaa ya Kigoma ujiji.

Sanjari na hayo baraza la madiwani limesema kuna baadhi ya wabadhilifu wamesharejesha fedha huku wengne wakishushwa vyeo vyao pamoja na kuwapeleka katika vyombo vinavyohusika ili iwe fundisho kwa wengine.