Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye ni kama amekalia kuti kavu katika nafasi yao.
Hali hiyo inatokana na kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa leo Alhamisi Januari 23, Ukonga jijini Dar es Salaam wakati akizindua nyumba za askari magereza.
Magufuli ameitaja wizara hiyo kuwa inamtesa sana hasa katika mikataba mbalimbali ambayo mara nyingi imekuwa ikiundiwa tume hususani mkataba wa Euro milioni 408 wa hivi karibuni ulioingiwa na wizara hiyo na Kampini ya Romania.
"Nasema kwa dhati, Kamishana Jenerali Andegenye nampenda sana ni mchapakazi lakini kwenye hili hapana, nilitegemea hapa awe hayupo". alisema Rais Magufuli.
“Hatuwezi kuendesha nchi kwa misingi ya ajabu namna hii, yanayokwenda kununuliwa mule kwenye mkataba ni ya ovyo mara drones… ni ya ajabu na ndiyo maana nampongeza Meja Jenerali Kingu, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kuwajibika na hii imempa heshima kwamba angalau ametambua kwamba inawezekana haya hakuyafanya yeye lakini kwa sababu yeye ni katibu mkuu amewajibika kwenye hilo. Ninampongeza sana na nitaendelea kumheshimu sana.
“Lakini nakueleza Lugola na Kamishna Jenerali, ninawashangaa kuwaona mko hapa… ninakupenda sana lakini this is the fact (huu ndiyo ukweli), sitaki kuwa mnafiki trilioni moja na kitu mtu anasaini wakati sheria zote zinajulikana wizara zote mwenye mamlaka ya kukopa ni wizara ya fedha aliendelea kusema Rais Magufuli.
Ikiwa hivyo basi kila wizara itakuwa inakopa hata mimi nitakiopa.
“Sasa mimi nitaendelea kuwapenda lakini kwenye position (nafasi) hii no (hapana),” amesema Rais Magufuli.