F Mama Shadya karume aziomba Taasisi binafsi kusaidia watoto wa kike Nchini | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mama Shadya karume aziomba Taasisi binafsi kusaidia watoto wa kike Nchini



Na Thabit Madai,Zanzibar.

Mlezi wa Mtandao wa kuwasaidia watoto wa kike kupata maendeleo ya Elimu (FAWE)  Zanzibar Mama Shadia Karume amezitaka Jumuiya zisizo za kiserekali kuwasaidia watoto wa kike  wanaoishi katika mazingira magumu ili kufikia malengo waliojiwekea.

Mama Shadya Karume aliyasema hayo huko Haileselassie  Mjini Unguja  wakati akifungua Mkutano wa Tisa  wa Jumuiya hiyo.


 Alisema kwamba  kumpatia elimu mtoto wa kike ni msingi mzuri katika kulinda familia hivyo ni muhimu taasisi za kiraia kushirikiana na Serikali kuwapatia  elimu hasa masomo ya Sayansi na Teknolojia ili waweza kujitegemea  na kujikwamua katika  hali ngumu yamaisha.

Aidha alisema  kuwa program ya Tuseme ni muhimu sana kwa  wanawake  kwani inawafanya watoto wa kike  kujiamini na kuwasaidia katika kujieleza kuwa yeye ni nani na anataka nini .

Mama Shadia aliongeza kuwa masomo ya Sayansi yanawasaidia vijana kiuchumi na kijamii hivyo ameipongeza Jumuiya ya FAWE kwa kuanzisha program ya Stemp kwa wanaume na wanawake.

Mama Shadya alizishauri Taasisi za Kiraia kuisaidia Jumuiya hiyo na kuwataka vijana kujiunga na FAWE ili waweze kunufaika  na elimu inayotolewa.

Mratibu wa Jumuiya ya FAWE Hinda Abdallah Ajmy alisema  kuwa wameamua kuwashirikisha watoto wa kie wengi zaidi kuliko wanaume kutokana na woga walionao na itahakikisha inawasaidia kuwajengea uwezo wa kujiamini.

Alisema wamekuwa wakitoa ushauri kwa Wizara  ya Elimu ili kuhakikisha kuwa mtoto wa kike anasaidiwa kupata elimu hata wale ambao uwezo wao wa kusoma ni mdogo kutokana na mazingira yasiyorafiki ya maisha.

Aidha alifahamisha kuwa wameanzisha mradi wa fadhili watoto mayatima   na kuwasaidia watoto zaidi ya 200 wanaishi katika mazingira magumu wanume na wanawake Unguja na Pemba.

Mwenekiti wa Jumuiya hiyo Dkt, Mwatima Abdallah aliwaomba viongozi waliochaguliwa kuendelea kuwa na moyo wa kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili na wao wapate elimu.

Akitoa ushuhuda, mwanafunzi Amina Omar Kitwana kutoka Klabu ya Tuseme alisema  kuwa mafunzo aliyopatiwa yamemsaidia kuwa na uwelewa kuweza kujiamini popote.

Sambamba na hayo wanafunzi ambao wamefadhiliwa kimasomo na FAWE wameahidi kuyafanyia kazi waliyoyaahidi wakati walipotaka ufadhili huo.

Fawe imenziswa mwaka 1998 na ina wanachama 140 kutoka Unguja na Pemba ambapo Kauli mbiu ni FAWE ZANZIBAR KUWA KARIBU NA WASHIRIKI WA MAENDELEO KUMUENDELEZA MTOTO WA KIKE KIELIMU.