F Mbeya: RC Chalamila kuhakiki madhehebu ya dini | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mbeya: RC Chalamila kuhakiki madhehebu ya dini

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema atatangaza zoezi la uhakiki wa Madhehebu ya Dini yaliyomo ndani ya Mkoa wa Mbeya ili yanayokiuka taratibu na Sheria yafungwe.

Amesema Jiji la Mbeya linakadiriwa kuwa la pili Afrika kwa kuwa na Madhehebu mengi lakini bado ni miongoni mwa Majiji yenye matukio mengi ya ajabuajabu.

Amesema baadhi ya Madhehebu hayo yanakiuka taratibu na tayari Ofisi yake imeanza kupokea malalamiko kwamba baadhi ya Madhehebu yameanza kuhatarisha amani na utulivu unaoendelea ndani ya Mkoa huo.