Na Amiri kilagalila-Njombe.
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Majengo halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wamekosa makazi baada ya mvua yenye upepo mkali kunyesha na kuezua mapaa ya nyumba zao na nyingine kubomoka kuta.
Waathiriwa hao akiwemo Rehema Ngonjera , Kaimery Godwin wanasema kuta zimeanguka na mapaa mengi kuezuliwa kwasababu ya upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyonyesha .
Madhara mengine ni kuharibiwa kwa miundombinu ya barabara na mazao mashambani jambo ambalo limeanza kuleta shaka endapo watapata mazao ipasavyo huku pia wakiomba serikali kuona namna ya kuzisaidia kaya za wazee na zisizojiweza.
“Zimeezua paa na wengine kuta zimeenguka kwa hiyo maafa yamekuwa makubwa sana sio hilo tu hata mtoni humo mazao,mifereji imeharibika atthari ni nyingi sana kwa ninaomba viongozi wa serikali wajaribu kuliangalia hili”
Akitoa ufafanuzi wa awali kuhusu athari zilizotokea mwenyekiti wa mtaa wa Majengo Edson Filangali anasema takribani nyumba 17 zimeezuliwa paa na kuta kuanguka huku akitoa rai kwa wananchi wa mitaa hiyo kuendelea kuwasaidia wahanga hao.
“Niwaombe tu wananchi tusaidiane kwenye hili na hawa ambao nyumba zao zimeezuliwa hawakupenda iwe hivyo,kuna wengine nguo zimeharibika kwa hiyo yule atakayesikia ngoma atoe kile kitakachomsaidia mwenzake”alisema Edson Filangali
Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Njombe EMMANUL GEORGE ambaye amefika katika eneo la tukio amewataka wananchi kushirikiana na serikali katika kuwasaidia wahanga hao ambapo ametoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kuchukua tahadhali kwa kukagua nyumba zao na kuzifanyia marekebisho mapema.
“Jukumu la serikali ni kutambua lakini pia kusaidia kwa pamoja sisi na wananchi kuhakikisha wale wenzetu ambao wamepata maafa haya kuwasaidia na kuweza kuwaludisha kwenye hali zao ili wendelee na uzalishaji,kwa wale wenye mahitaji ya haraka tumeweza kuweka miundombinu ya kuweza kuwasaidia kwa haraka lakini pia serikali itatoa mchango na wananchi pia tumewaomba wachangiane kama waafrika tunavyoishi”
Aidha katibu tawala amesema serikali imetoa angalizo kipindi hiki cha mvua na upepo wananchi ambao nyumba zao zina hitilafu waweze kurekebisha kuliko kusubiri maafa.