Na John Walter-Babati-Manyara
Watoto wawili wanaosoma darasa la pili katika shule ya Msingi Maisaka kata ya Maisaka wilaya ya Babati mkoani Manyara, wamelawitiwa na mtu ambaye bado hajafahamika na kusababishiwa maumivu katika Miili yao.
Uchunguzi uliofanywa na wataalamu katika Hospitali ya mji wa Babati (MRARA) umebaini kuwa watoto hao wamefanyiwa kitendo hicho cha kikatili.
Taarifa kutoka kwa Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Manyara Paul Kasabago,imeeleza mtuhumiwa huyo aliwachukua watoto hao wenye umri wa miaka 7 na 8 wakiwa njiani kuielekea shuleni na kuwarubuni kuwapa pesa kiasi cha shilingi 500.
Kamanda Kasabago amewaambia waandishi wa Habari kwamba walioufanya umebaini kuwa mtu huyo aliwachukua na kuiwapeleka eneo la Makaburi ya Mruki na kuwalawiti kwa zamu baada ya kuwatishia kuwaua endapo wasingetekeleza matamanio yake.
Juhudi za kumtafuta na kumkamata mtuhumiwa zinaendelea na mara tu atakapokamatwa atafikishwa Mahakamani.