F Mimba mashuleni wilayani Rorya zafikia 117 kwa mwaka 2019/2020 | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mimba mashuleni wilayani Rorya zafikia 117 kwa mwaka 2019/2020


Na Timothy Itembe, Mara.

MIMBA mashuleni wilaya Rorya mkoani Mara kwa mwaka wa fedha 2019/2020 zimefikia 117 huku shule za msingi zikiwa 13 na Sekondari 104.

Mganga mkuu wilaya Rorya,Peter Mkenda jana alisema katika Baraza la madiwani kuwa mimba mashuleni kwa mwaka wa fedha 2019/2020 zimefikia 117 huku katika shule za msingi mimba zikiwa 13.

Mkenda aliongeza kuwa mimba mashuleni nichangamoto kwasababu baadhi ya wazazi hawana mwamko wa kutoa ushirikiano kwa vyombo vinavyohusika kutoa taarifa pamoja na ushahidi  ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

"Halmashauri yetu ni moja ya halmashauri hapa nchini zinazokumbwa na changamoto ya mimba mashuleni lakini chakushangaza ni pale ambapo wazazi hawana mwamko wa kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa pamoja na ushahidi kwenye  vyombo vinavyohusika ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria"alisema Mkenda.

Mkenda  alitolea mfano wa kesi Namba TRR/CID/SCR/652/2019 iliyopo katika mahakama ya wilaya Tarime inayo mhusisha mtuhumiwa anayemtambua kwa jina moja tu Elikana ambaye ana Zahanati Bubu katika kijiji cha Mwarango ambaye anatuhumiwa kumtoa mimba mwanafunzi wa darasa la Tano wa shule ya msingi Nyamagaro mwenye Umri wa miaka 15 na mkazi wa kijiji cha Kyangasaga ambayo inayumba  kwa kukosa ushahidi.

Kwa upande wake diwani kata ya Kyang'ombe kupitia Chama cha mapinduzi alitumia nafsi hiyo kutupia lawama Jeshi la Polis kuwa kusimama upande wa watuhumiwa na kuwashawishi wazazi wa mtoto waliopachikwa  mimba kumalizana kinyumbani.

Pia diwani huyo aliongeza kuwa baadhi ya wazazi wenye uwelewa mdogo wanashindwa kwenda kutoa taarifa na ushahidi kwenye vyombo vinavyohusika ili watuhumiwa watiwe hatiana.

Naye diwani viti maalumu kata ya Kitembe kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema,Mery Thomas alisema kuwa asilimia kubwa ya mimba mashuleni na mimba za umri mdogo zinawatesa wazazi na watoto upande  wa watoto wa kike kwani mimba hizo zinazima matarajo ya ndoto za maisha kwa  watoto wa kike tofauti na watoto wa kiume.

Thomas alifafanua kuwa wazazi na watoto wa kiume wanaopachika mimba watoto wa kike wao maisha kwao ni rahisi na ndio sababu wakati mwingine wanatumia garama kuyumbisha kesi kwa mazingira yeyote na hata kutumia fedha ili mabo yao yafanikiwe ambapo  mtoto wa kike yeye anafukuzwa shule na kuacha masomo kwa hali hiyo serikali iwachukulie hatua kali wale ambao wanawapa watoto wenye  umri mdogo miba ikiwemo wanafunzi wa kiume waliohusika kuwapa wanafunzi wenzao wa kike mimba wote wachukuliwe hatua zinazofanana ikiwemo ya kuachishwa  masomo  wote isichalishe wakiume au wa kike sheria isipendelee.

Mmoja wa wazazi Amos Mang'era mkazi wa mtaa wa Kinyambi kata ya Nkende alisema kuwa changamoto inayowakuba baadhi ya wazazi wenye watoto waliopata mimba ni pela ambapo wanazungushwa polisi na hata kutengenezewa mazingira ya kutoa rushwa mwisho pamoja na kesi kufutwa Mahakamani pasipo wazazi kushirikishwa.