Picha ya Mlima Kilimanjaro ambayo imeonekana 'kutrend' mitandaoni, imepigwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete ikionesha muonekano wa juu wa Mlima Kilimanjaro.
Dkt. Kikwete amesema kuwa picha hiyo ameipiga wakati akiwa njiani akitokea Nairobi kwenda Dar es Salaam, saa chache baada ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili nchini Kenya, Daniel Arap Moi.