F Wazee wa Mtama washindwa kuzuia hisia zao kwa Rais Magufuli | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wazee wa Mtama washindwa kuzuia hisia zao kwa Rais Magufuli



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dkt. Bashiru Ally akiendelea na ziara yake Mkoani Mtwara kuelekea jimbo la Ndanda kupitia jimbo la Mtama, wazee wameshindwa kuzuia hisia zao kwa Rais Magufuli kwa kuonesha nia ya kutaka kumchangia gharama za fomu za Urais mwaka 2020.

Akieleza kwa niaba ya wazee hao, Mbunge wa jimbo la Mtama Ndg. Nape Mosses Nnaye, ameleeza kuwa wazee wapo tayari na wamejipanga kumchangia gharama za fomu za Urais ili kuonesha mapenzi yao kwake kutokana na namna anavyowajali wazee na wananchi kwa ujumla, hivyo wanasubiri kibali kwa Katibu Mkuu.

Wameyasema hayo asubuhi ya leo tarehe 22 Februari, 2020 katika ufunguzi wa shina la Wakereketwa la Kambarage jimboni Mtama.


Katibu Mkuu pamoja na mambo mengine, akifafanua uamuzi huo wa wazee, ameeleza kuwa, nia yao ni njema na imekuwa matamanio ya wazee wengi kufanya hivyo kama wao wa Mtama, amepokea nia yao njema lakini kikubwa wao waendelee kumuombea Mhe. Rais afya njema ili awatumikie zaidi bila kuchoka.

Katibu Mkuu yupo Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, yenye lengo la kuendelea kukirejesha Chama kwa wanachama