Na Hamisi Abdurahmani, Masasi
CHAMA cha walimu (CWT) wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kisema kuwa bado kimeendelea kukabiliwa na changamoto kubwa ya kusimamia utekelezaji wa sheria ya malipo ya stahiki za walimu kwa wakati kutoka kwa mwajiri ikiwemo stahiki za uhamisho,matibabu na upandishwaji wa madaraja.
Hayo yalisemwa jana wilayani Masasi na katibu wa chama hicho wilaya ya Masasi,Agnes Saidi alipokuwa akizungumza na waandishi habari ofisini kwake kuhusu kuelekea uchaguzi wa Chama hicho ambao unatarajia kufanyika hivi karibuni.
Alisema chama cha walimu ni taasisi ambayo inahudumia idadi kubwa ya walimu nchini na ni wazi kuwa imekuwa ikitetea haki za walimu wanachama wake katika kuhakikisha wanapata haki zao za msingi kutoko kwa mwajiri wao.
Alisema kanuni ya utumishi wa umma imewaka wazi kuwa mwajiri anawajibu kumpatia stahiki zake mwajiri wake pale anapokuwa anamwamisha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Alisema lakini hadi sasa kanuni hiyo imekuwa na ukakasi kwa mwajiri katika utekelezaji wake hivyo wapo baadhi ya walimu wamekuwa wakihamishwa lakini kupata stahiki zao kwa wakati imekuwa changamoto kubwa inayoitafuna chama cha walimu kuishughulikia.
Saidi alieleza kuwa wapo baadhi ya walimu ambao walitakiwa kupatiwa stahiki zao za matibabu lakini nazo zimekuwa ni changamoto kuzipata kwa wakati hivyo kama chama cha walimu kimeendelea kuhakikisha stahiki zao zinataolewa kwa wakati ili walengwa waweze kupata haki yao ya msingi.
“Kanuni na sheria inasema kuwa mwajiri anapotoa uhamisho ni lazima atowe stahiki yake kwa yule aliyempa uhamisho lakini hadi sasa sheria hii kwa mwajiri imekuwa ngumu kuitekeleza hivyo walengwa wengi wamekuwa hawapati stahiki zao kwa wakati tunaiomba serikali iliangile hili kwa kina,”alisema Saidi
Alisema changamoto nyingine ambaye wao kama CWT wanaendelea pia kupambananayo ili kuhakikisha wanachama wake wanapata haki zao ni pamoja na stahiki za upandaji wa madaraja na zo zimekuwa shida kupatikana kwa wakati.
Saidi alisema mwalimu anapopandishwa daraja ni wajibu alipwe stahiki za kupanda daraja lakini bado utekelezaji huo umekuwa ni mgumu pia mwa mwajiri hivyo kesi hizo zimekuwa ni mara kwa mara kwa chama cha walimu.
Alisema CWT pia kimebaini kuwa walimu wenyewe kushindwa kutambua haki zao za msingi pamoja na kutombua jinsi ya kufuatilia hali ambayo inachangia kuwepo kwa malalamiko mengi ya walimu kutolipwa stahiki zao kwa wakati.
Alisema hivyo kutokana na hilo chama hicho pia kimekuwa kikitoa elimu na maelekezo kwa wanachama wake kufahamu njia sahihi za kufuatilia stahiki zao ambazo mwajiri anapaswa kuzitoa kwao.