F Dkt. Kalemani aagiza wakuu wa mikoa na wilaya wapewe orodha ya vijiji vinavyosambaziwa umeme wa REA ndani ya siku 10 | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Dkt. Kalemani aagiza wakuu wa mikoa na wilaya wapewe orodha ya vijiji vinavyosambaziwa umeme wa REA ndani ya siku 10

Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa kusambazaji Umeme Vijijini(REA) wameagizwa kutoa orodha ya vijiji wanavyosambaziwa umeme kwa Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa ndani ya mwezi huu ili viongozi hao watoe majibu ya uhakika kwa wananchi.


Hayo yamebainisha na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma.

Dkt.Kalemani amesema kuwa kila mkandarasi anatakiwa kuwasilisha mpango kazi wa kufikisha umeme maeneo ambayo bado hayajafikiwa kwa viongozi hao ndani ya mwezi huu ili watoe majibu kwa wananchi pindi watakapotaka kujua lini watapatiwa umeme maeneo yao.

“Hili litasaidia viongozi hao kuwapatia majibu sahihi wananchi wao wanao waongoza iwapo yatatokea maswali ya kutaka kufahamu ni lini watafikiwa katika kupatiwa umeme”amesema Dkt. Kalemani

Aidha, Dkt.Kalemani amesema kuwa nguzo ambazo zimewekwa chini  katika maeneo yao ya kazi zisimamishwe sambamba na kufunga transfoma na kukaza  nyaya zilizolala ndani ya mwezi huu zoezi hilo liwe limekamilika

Dkt.Kalemani amesema kuwa  mkandarasi na msimamizi wa mradi atakayeshindwa kufuata maelekezo hayo atachukuliwa hatua stahiki kwa kuwa wananchi wanataka umeme ili kuongeza chachu ya maendeleo.

Ameongeza kuwa serikali imetenga fedha za kutosha na kwa mwaka wa bajeti 2019/20 unaomalizika juni mwaka huu Sh.Bilioni 492 kwa ajili ya kupeleka umeme vijiji zaidi ya 3599.

Dkt.Kalemani amesema mpaka sasa Vijiji 91,000 vimepatiwa umeme ndani ya miaka nne ya serikali ya awamu ya tano ambapo inaongeza chachu ya mafanikio makubwa katika kuelekea uchumi wa kujenga viwanda.

“Sisi kama wizara ni jukumu letu kusimamia usiku na mchana kufikisha umeme katika vijiji taklibani 20,800 ambao hawajapatiwa umeme ndani ya miaka miwili ijayo sasa,” amebainisha Dkt. Kalemani

Ameongeza “Katika mpango unaoendelea tumebakiza vijiji 1822 vijiji hivi vitaanza kupelekewa umeme kuanzia mwezi juni mwaka huu ili ifikapo mwakani juni viwevimepatiwa umeme.Kwa sasa tuna tekeleza miradi minne katika Mikoa ya Dar es salaam na Pwani ambapo kwa sasa tunasambaza umeme katika maeneo ya majiji, manispaa, ambayo kimsingi ni maeneo ya mitaaa ambayo kwa sura ukiyatazama ni sawa na sura ya vijijini(pedurban) nusu vijiji nusu mitaa.”

Amebainisha wameanza na miradi mitano maeneo yote yaliyoko pembezoni mwa majiji Dar es salaam ni   Kigamboni, Ilala, Mkuranga, Kibaha ,Bagamoyo, Chalinze, Kisarawe, Chanika na maeneo mengine na gharama za kuunganishiwa umeme kwa kila mtanzania Tsh.27,000.

 “Nitoe wito kwa wananchi kuvuta Subira katika maeneo yao tutawafikia kutokana na utaratibu huu, pia watupe ushirikiano kwa kuanza kufanya wayalingi katika majumba yao ili pale wakifikiwa wawewasha kamilisha kila kit una malipo ya kuunganishiwa Pia kulinda miundombinu , kama kutoiba transifoma na nyaya za umeme zitakazo fungwa katika maeneo yao,” amesema Dkt. Kalemani