F Idara ya uvuvi yakusudia kuboresha makazi ya wavuvi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Idara ya uvuvi yakusudia kuboresha makazi ya wavuvi



Na Thabit Madai,Zanzibar.

Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Zanzibar chini ya Mradi wa usimamiazi wa Shughuli za uviuvi kanda ya kusini Magharib mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH) imekusudia kurekebisha makazi ya Wavuvi katika kisiwa cha Pungume kilichopo wiliaya ya Magharib ‘B’ Unguja.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Doria kutoka Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Zanzibar, Haji Shomari Haji wakati akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kufanya Doria katika hifadhi ya Ghuba ya Menai.

Doria hiyo ilikuwa na lengo la kuangalia usalama wa wavuvi pamoja na uhifadhi wa mazingira katika maeneo ya bahari.

Mkuu huyo wa Doria alisema kwamba Idara ya maendeleo ya Uvuvi inatekeleza mradi wa usimamimizi wa shughuli zote za Uvuvi kanda ya kusini Magharib mwa bahari ya hindi ambapo moja kati ya   jambo ambalo wanatekeleza katika mradi huo ni kuboresha makazi ya wavuvi katika kisiwa cha Pungume.

“Tulipoanza kutekeleza mradi huu tulianza na kutengeneza ofisi za Doria Idara katika kisiwa hichi na maeneo mengine hivyo sasa tumekusudia kuboreha maazi ya wavuvi hususani wale wanaokaa kwa muda mrefu (Dago),” alisema Mkuu huyo wa Doria Haji shomari Haji.

Alisema matengenezo ya ofisi za Idara ambazo zitakuwa zinasimamia Doria zimeshakamilika pamoja na ununuzi wa Boti mbili za kisasa ambazo zote zinafanya kazi ya Doria na uwokozi.

“Si kukagua tu shughuli za uvuvi bali tunafanya na uwokozi tukishirikiana nKMKM katika maeneo ya bahari” aliongeza Kusem Mkuu huyo wa Doria.

Mkuu huyo wa Doria akizungumzia Doria ambayo waliifanya walifanya katika eneo la Ghuba ya Menai, alisema kwamba lengo la Doria hiyo ilikuwa ni kuangalia shughuli nzima za uvuvi pamoja na kuangalia kwa namna gani utaratbu uliwekwa unafuatwa.

Pia alisema kwamba katika doria hiyo ilikuwa na lengo la kuangalia namna ya wavuvi wanavyovua kwa usalama na kulinga mazingira ya bahari.

“Shughuli za uvuvi kama hazitasimamiwa ipasavyo basi hakutakuwa na usalama baharini lakini pia hautakuwa na utunzaji mzuri wa Mazingira” alisema Mkuu huyo wa Doria.

Aidha alieleza kwamba changamoto ambazo wanakabiliana nao katika shughuli zao la Doria ni wavuvi ambao hufanya shughuli uvuvi bila ya kuwa leseni ya shughuli hiyo.

“Leseni ya uvuvi huwa inapatiana kwa bei rahisi na hupatikana kwa urahisi lakini wavuvi baadhi ya wavuvi wanashindwa kuonesha ushirikiano kwa kukata leseni ya shughuli zao” alieleza Mkuu huyo wa Doria.

Aliongeza kueleza kwamba pindi wanapowakamata wavuvi ambao hawana vibali katika kazi yao huwa wanawasitisha kuendelea kazi ya uvuvi kwa muda ule ili wakafanye taratibu za kukata leseni na kundelea na shughuli zao za uvuvi.

 “Ukiwakuta baharini na ukiwaacha waendelee kuvua basi hawataka leseni maana wanaambizana kuwa hata wakikutwa basi huachwa kuendelea na shughuli zao” alieleza Mkuu wa Doria.

Kwa upande wa Wavuvi walipongeza hatua zinazochukuliwa na Idara ya vuvi kwa kuwasimamia Shughuli zao ili wasiiuke mipaka pamoja na kulind mazingir ya Bahari.

Mshenga Mgeni Mvuvi wa ngisi katika eneo la kisiwa cha Pungume alisema kwamba Idara ya maendeleo ya uvuvi ambao wanatekeleza mradi SWIOFISH wameuwa wakiwasimamia vizuri shughuli zao.

“Idara wamekuwa wakija hapa kutupa maenelekezo namna ya kuvua pamoja na kutuongoza namna ya kulinda mazingira lakini pia tumesikia kuwa wanatutengeza vyoo katika maeneo yetu ya Dago,” alisema Mshenga Mgeni Mvuvi wa Ngisi.

Nae Juma Othamin Mvuvi alieleza kwamba kwa sasa wao kama wavuvi wanavua katika maeneo salama chni ya uangalizi wa Idara.

“Tumepewa eneo la kujihifadhi katika kisiwa hichi cha Pungume ambapo tunapokwenda kuvua na tunasehemu salama ambayo tunajihifadhi sisi pamoja na vyombo vyetu” alieleza Mvuvi huyo.

Mradi wa usimamiazi wa Shughuli za uviuvi kanda ya kusini Magharib mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH) ni mradi wa miaka 6 ambapo unajumuisha nchi tatu, Tanzania,  Comoro na Msumbiji na  unafadhiliwa na Benk ya Dunia.