F Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kuzifungia shule kwa muda usiojulikana | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza kuzifungia shule kwa muda usiojulikana



Na Thabit Madai,Zanzibar.

Kufuatia hali ya Mripuko wa virusi vya corona,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetangaza kuzifunga  shule zote za maandalizi, Msingi, Sekondari,Madrasa za qurani pamoja na vyuo vikuu kwa muda usiojulikana.

Pia Serikali  inazuia mikusanyiko inayokutanisha watu wengi kwa wakati mmoja ikiwemo mikutano, makongamano, semina, warsha, michezo ya ligi kuu, ligi za kanda, burudani za ngoma pamoja na shughuli za harusi.

Tamko hilo lmetolewa  na Waziri wa Afya Zanzibar,Hamadi Rashid Mohamed wakati akizungumza na Waandishi wa  Habari  katika ukumbi wa Wizara ya Habari na mambo ya kale Zanzibar iliyopo kikwajuni mjini Unguja.

Waziri huyo alisema kwamba Serikali  imechukua hatua hiyo kutokana na hali ya mripuko wa Virusi vya Corona ambapo kwa sasa  mgonjwa mmoja amebainika na maradhi hayo  kati ya wagonjwa watatu ambao wameshukiwa kuwa na maradhi hayo.
                           
“Hapa kwetu Zanzibar, siku ya  tarehe 17 Machi, 2020, tulipata washukiwa watatu wa ugonjwa huo, wawili wakiwa ni raia wa kigeni ambae ni Mghana na Mjerumani na mwengine ni Mtanzania, Watu wote hao watatu walikuwa na dalili ya ugonjwa huo na kama ilivyo kawaida hatua zilichukuliwa za kuchukua sampuli kwa uchunguzi wa kimaabara,”alieleza Waziri huyo.

Aliongeza kuwa Alfajir ya  march 18 walipokea majibu ya sampuli hizo ambapo kwa bahati mbaya mmoja kati ya hao amekutwa akiwa ameathirika na maambukizo ya kirusi cha COVID 19 ambaye ni Raia wa Ghana aliyeingia nchini kutokea Ujerumani na Shirika la Ndege la Kenya Air way tarehe 11/3/2020 muda wa saa 3:20 asubuhi. Mtu huyo ni mwanamme mwenye umri wa miaka 24.

 Alifahamisha  kuwa Kwa sasa, mgonjwa huyo amelazwa katika kituo maalum kilichotengwa kwaajili ya maradhi ya mripuko huko Kidimni wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Waziri aliongeza kueleza kuwa Serikali  inawataka watu wote wanaoingia nchini kutoka nchi zilizoathirika na maradhi hayo kufuata utaratibu wa kujitenga kwahiari kwa muda wa siku 14 kwa gharama zao wenyewe pamoja na kufuatamasharti ya afya.

 “Serikali inakataza na inakemea vikali utumiaji wa bandari zisizorasmi kwa ajili ya kuchukua abiria na mizigo hivyo watu wotewanatakiwa kutumia babdari rasmi, kama vile bandari ya Malindi,Mkokotoni kwa upande wa Unguja na Mkoani, Wete na Wesha kwa upande waPemba. Hata hivyo vyombo vitakavyotumika nje ya bandari zilizorasmi,”alieleza Waziri huyo

Alisema Serikali inazuia safari zote za nje ya nchi kwa watendaji wake napia kwa wale watakaokuwa na ulazima wa kusafiri wanapaswa kuchukuahatua za kujilinda na maradhi hayo. Aidha, Serikali inawashauriwananchi kwa wakati huu kuepuka safari zisizo za lazima za nje ya Zanzibar.

Hata hivyo  alisema kuwa Serikali inalaani vikali vitendo vya wafanyabiashara kutumia ugonjwa huu kwa faida zao kwa kupandisha bei za vifaa vya kinga, bidhaa na huduma nyengine na hatua kali zitachukuliwa kwawatakaobainika kufaya hivyo na tayari taasisi ya kumlinda mlaji imepewa agizo la kufuatilia suala hilo.
         
Katika hatua nyingine Waziri huyo alisema Serikali inawataka wananchi wote kuacha kusikiliza taarifa zisizorasmi na badala yake wasikilize taarifa rasmi zitakazotolewa naSerikali. kusiKiliza utaratibu na taarifa zitakazotolewa na Serikalijuu ya mripuko wa maradhi hayo ambazo zitakuwa zikitolewa mara kwamara.

Aidha aliwashauri wananchi wanaokwenda masokoni na maeneo mengineya kutafuta huduma kuepuka mikusanyiko na baada ya kupata huduma na warudi majumbani pia Serikali inawataka wananchi kupunguza msongamano katika hospitali  badala yake watu wasiozidi wawili wataruhusiwa kumuona mgonjwakwa siku na inashauriwa wananchi watumie vituo vya afya vilivyokuwakaribu nao ili kuepuka msongamano katika hospitali kuu.

Hadi sasa Zaidi ya nch 160 zimesharipoti uwepo wa virusi vya corona ambapo kwa bara la Afrika zaidi ya nchi 25 ikiwemi Tanzania imeripoti kuwepo kwa virusi hivyo vya corona.