F Watanzania 9 wazuiwa kuingia Uganda | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Watanzania 9 wazuiwa kuingia Uganda

Agizo la Rais wa Uganda, Yoweri Museven kuzuia wageni kuingia katika nchi hiyo ili kuondoa uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi ya corona limeanza na wafanyabiashara tisa wa Tanzania ambao wamerudishwa nyumbani chini ya usimamizi wa polisi ikiwa ni utekelezaji wa agizo hilo.

Polisi nchini Uganda imewataja wafanyabiashara hao waliopitia bandari ya Mwanza kwa kutumia MV Upendo kuwa ni Juma Mahalaganya, Kondo Msrika, Spencer Jupinya, Hajji Juma, Matthias Alistens, Siraje Kasiim, Mussa Alfari, Raphael Abel na Malizia Osward.

Msemaji wa polisi nchini Uganda, Fred Enanga amesema leo Jumatatu Machi 23, 2020 hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Museveni la kufunga maeneo yote ya mpaka wa Uganda.

"Tuna nchi ambayo iko salama sana. Vyombo vya usalama vya pamoja vinahakikisha hakuna mtu anayeingia Uganda; pamoja na watembea kwa miguu, wapanda baiskeli au madereva,"alisema.
Ofisa huyo wa polisi amesema kuwa usalama katika maeneo yote ya mpaka wa Uganda ulinzi umeimarishwa kwa lengo kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa corona.

Vilevile alisema pande za kusini zilizopakana na Rwanda na Tanzania pia ulinzi umeimarishwa.
Ameongeza kuwa timu ya pamoja ya usalama sasa inatilia mkazo katika kutekeleza marufuku ya kusafiri kwenda na kutoka Uganda na kuhakikisha hakuna watu wanaoingia nchini Uganda kwa kutumia  ardhi au maji.

Rais Museveni aliamuru kufungwa kwa mipaka yote na kusimamisha ndege za abiria masaa machache kabla ya Uganda kuthibitisha kisa chake cha kwanza cha virusi vya corona.

Mgonjwa aliyepatikana na virusi vya corona nchini Uganda ni mfanyabiashara wa Uganda ambaye alikuwa amesafiri kwenda Dubai Machi 17, 2020 na akarudi Machi 21