F Baada ya kumwagana na Mnigeria Gigy Money atamani kufa "Siwezi kula wala siwezi kulala" | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Baada ya kumwagana na Mnigeria Gigy Money atamani kufa "Siwezi kula wala siwezi kulala"

Mapenzi yananguvu kubwa hii imejionyesha kwa mrembo wa tasnia ya filamu na muziki Gigy Money baada ya kumbebesha virago Mpenzi wake Mnigeria ameeleza kwamba anatamani kufariki Dunia, kwa sababu anaona hawezi kula wala hawezi kulala.

Kupitia post aliyoweka katika mtandao wa kijamii wa Instagram Gigy Money amesema, hawezi kuamini kinachomtokea, anaona anajichukia mwenyewe na amekuwa dhaifu.

"Natamani kufariki bila sababu yoyote, siwezi kula wala siwezi kulala kwa kifupi siamini na hii imezidi, sasa najichukia mimi mwenyewe na nimekuwa dhaifu, yaani inauma ila inabidi uwe mkubwa kuelewa, sipo "interested" na mtu yeyote yule wote wamenishinda nimechoka" ameandika Gigy Money.

Aidha kwenye comments za post hiyo Gigy Money ameonesha kuyalalamikia mapenzi, hii imekuja baada ya kupita siku mbili tangu kugombana na mpenzi wake raia wa Nigeria Hunchy Huncho, ambaye alimfukuza nyumbani kwake.